TUME YA UCHAGUZI YATEUA MRITHI WA DK. ELLY MACHA
Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Catherine Nyakao Ruge |
Na Mtapa Wilson
Tume ya
Taifa ya uchaguzi leo imemteua Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge wa wa Viti
Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Catherine anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum akiwakilisha walemavu
kupitia Chadema, Dk. Elly Macha, ambaye alifariki mwishoni mwa mwezi Machi katika
hospitali ya New Cross, Wolverhamton nchini Uingereza, ambako alikuwa akitibiwa.
Kabla ya
kuteuliwa kwake Catherine alikuwa mwanaharakati na masuala ya jinsia na haki za
binadamu. Lakini pia ni muweka hazina wa
Chadema kanda ya Serengeti, nafasi ambayo anaishikilia mpaka sasa.
TUME YA UCHAGUZI YATEUA MRITHI WA DK. ELLY MACHA
Reviewed by Unknown
on
17:36
Rating:
No comments: