MBUNGE ALIYEFUNGWA JELA AACHIWA HURU
Mbunge wa Jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijuakali. |
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam, leo imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali.
Katika kesi ya msingi, Mbunge huyo wa Kilombero, amekutwa hana hatia baada ya kutumikia kifungo jela kwa takribani miezi miwili na nusu.
Januari 11, mwaka huu, hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Timothy Lyon, alimuhukumu Lijuakali, kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Hakimu Lyon alisema kuwa Mahakama ilimtia hatiani kwa kosa hilo kwa kuwa Lijuakali alikuwa na kesi tatu huko nyuma ambazo alitiwa hatiani na kuhukumiwa ikiwemo kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014.
MBUNGE ALIYEFUNGWA JELA AACHIWA HURU
Reviewed by Unknown
on
09:50
Rating:
No comments: