KILICHOSABABISHA SOPHIA SIMBA NA WENZAKE KUFUKUZWA CCM
Takribani siku nne zimepita tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua maamuzi ya kuwafukuza wanachama wake kwa tuhuma za usaliti wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni mwa wanachama waliofukuzwa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Sophia Simba na Wenyeviti wa mikoa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti moja leo limetaja sababu zinazodaiwa haswaa kusababisha vigogo hao wa siasa ndani ya chama tawala kufukuzwa uanachama.
Taarifa inasema kuwa Sophia Simba yeye anadaiwa kuwa hata baada ya uchaguzi mkuu, yeye aliendelea kwenda nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA, Edward Lowassa, kwa kificho akiwa kavaa hijabu, na hivyo kudaiwa kuwa amekuwa akipeleka siri za chama kwa Lowassa.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya. |
KILICHOSABABISHA SOPHIA SIMBA NA WENZAKE KUFUKUZWA CCM
Reviewed by Unknown
on
19:39
Rating:
No comments: