TBC YAWASIMAMISHA KAZI WATANGAZAJI TISA KWA KURUSHA HABARI YA UONGO
Na Mwandishi wetu
Menejiment ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) imewasimamisha
kazi watangazaji tisa wa shirika hilo, ambao walirusha hewani taarifa ya uongo kuwa
Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli
na kwamba ni mfano mzuri wa kuigwa barani Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo na gazeti la
Mwananchi, Mtendaji wa TBC, Dk. Ayub Rioba amethibitisha taarifa hiyo na kuwataja
waliosimamishwa kazi kuwa ni Elizabeth Mramba, Gabriel
Zacharia, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani
Mpenda, Leah Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.
TBC ilitangaza habari hiyo ya uongo baada ya kuinukuu kutoka katika mtandao wa 'Fox-chanel.com', ambao unaodaiwa kuchapisha taarifa za uzushi kwa ajili ya kujipatia manufaa ya kibiashara na kufanya propaganda.
Mtandandao huo umewahi kuripoti kuwa Rais wa Zimbabwe,
Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Lakini pia hivi karibuni mtandao huo uliripoti taarifa nyingine ya uzushi kuwa Rais Magufuli amewataka wananchi wa nchi jirani ya Kenya
kumuondoa madarakani Rais Uhuru Kenyatta, kwa madai ya kuwa utawala wake unawapeleka
matatizoni.
TBC YAWASIMAMISHA KAZI WATANGAZAJI TISA KWA KURUSHA HABARI YA UONGO
Reviewed by Unknown
on
10:54
Rating:
No comments: