ACACIA YAKATAA KUILIPA TANZANIA DOLA BILIONI 180
Mgodi wa Buzwagi uliopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga. |
Serikali ya Tanzania inadai deni hilo ambalo linasimamia mapato yaliyopatikana na hayakutajwa kutoka katika migodi miwili ya Buryanhulu na Buzwagi Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga katika kipindi cha mwaka 2000 na 2017.
Acacia ambayo ndio kampuni kubwa inayoongoza kwa uchimbaji wa madini nchini Tanzania imesisitiza kuwa imekuwa ikitangaza taarifa zake za mapato kila mara.
Taarifa hiyo imekuja kipindi ambacho tume mbili za Rais wa Tanzania, John Magufuli, ambazo zilichunguza masuala ya madini ikiwemo kiwango cha madini kilichomo kwenye mchanga unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kuishutumu Acacia kufanya kazi zake kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kukwepa kulipa kodi.
CHANZO: BBC
ACACIA YAKATAA KUILIPA TANZANIA DOLA BILIONI 180
Reviewed by Unknown
on
17:13
Rating:
No comments: