TUNDU LISSU APATA DHAMANA
Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. |
Na Mtapa Wilson
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana
mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kinyume na maombi yaliyowekwa na
mawakili wa Jamhuri ya kuzuia asipewe dhamana.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri amesema kuwa baada
ya kupitia hoja za serikali na majibu ya mawakili wa utetezi, haoni mantiki ya
kuzuia dhamana kwa Lissu.
Hivyo mahakama hiyo
imemuachia Lissu kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya
shilingi milioni 10 kila mmoja.
TUNDU LISSU APATA DHAMANA
Reviewed by Unknown
on
08:59
Rating:
No comments: