GWAJIMA ATANGAZA MAOMBI MAALUMU KWA TUNDU LISSU
Mchungaji wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini, Josephat Gwajima, amesema jumapili wiki hii
ataongoza maombi maalumu kwa ajili ya kuombea afya ya Tundu Lissu na kulaani
vikali shambulio la risasi lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi yake.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Gwajima imesema kwamba maombi hayo yatafanyika kanisani
kwake Ubungo jijini Dar es Salaam na
kuwaomba wananchi wengine kuungana nae katika maombi hayo.
“Jumapili hii tarehe
10/09/2017, nitaongoza maombi maalumu ya kuombea afya ya Mheshimiwa Tundu Lissu
na kulaani vikali kitendo cha kikatili na kinyama alichofanyiwa…..,” imesema
taarifa hiyo.
GWAJIMA ATANGAZA MAOMBI MAALUMU KWA TUNDU LISSU
Reviewed by Unknown
on
16:02
Rating:
No comments: