AFCON 2017: MISRI YAILAZA GHANA, MALI NA UGANDA WAAGA MICHUANO
Mohamed Salah |
Na Mtapa Wilson
Michezo miwili
imeshakwimalizika iliyokuwa inazikutanisha timu za Mali dhidi ya Uganda na
Misri dhidi ya Ghana, ambapo katika mchezo wa Mali ambayo ilikuwa inalazimika
kuilaza Uganda na kutumai Misiri ipoteze kwa Ghana, umeisha kwa sare pacha ya kufungana magoli 1-1.
Lakini kwa
upande wa mchezo wa Misri na Ghana umemalizika kwa Misri kuilaza Ghana kwa goli
moja kwa bila, ambalo limetiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Misri,
Mohamed Salah, katika dakika ya 11.
Kwa matokeo
haya sasa, timu za Misri na Ghana zimefanikiwa kufuzu na hatua inayofuata ya
robo fainali na kuziacha timu za Mali na Uganda zikiaga michuano hiyo ya kombe
la Mataifa huru Afrika.
AFCON 2017: MISRI YAILAZA GHANA, MALI NA UGANDA WAAGA MICHUANO
Reviewed by Unknown
on
21:50
Rating:
No comments: