MOROCCO YAREJEA RASMI UMOJA WA AFRIKA
Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli akiwa na mgeni wake Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, wakati alipotembelea Tanzania Oktoba 24, 2016. |
Addis Ababa, Ethiopia
Jumuiya ya
Umoja wa Mataifa huru Afrika (AU) imeridhia kurejea kwa Morocco katika Jumuiya
hiyo baada ya kujiondoa takribani miaka 33 iliyopita kutokana na hatua ya AU
kutambua jimbo la Sahara ya Magharibi kuwa mwanachama wake.
AU inatambua
Sahara ya Magharibi kuwa ni jimbo huru ambalo pia ni mwanachama wake, lakini
Morocco imeendelea kusisitiza kuwa eneo hilo ni mkoa wake wa kusini.
Morocco imepigania
mpango wake wa kutaka kurejea tena AU mwaka uliopita, ambapo Mfalme wa nchi hiyo,
Mohammed VI, alitemebelea nchi kadhaa za Afrika ikiwamo Tanzania na kufanya
mazungumzo na wakuu wa nchi hizo, jambo ambalo lilielezwa kama njia ya kutafuta
ushawishi wa kurejea kwake katika Jumuiya hiyo.
Eneo la
Sahara ya Magharibi linaendelea kuwa eneo lenye utata mkubwa licha ya kuwa
Wakuu wengi wa nchi za Afrika wamepiga kura na kuikubali Morocco kurejea katika
Umoja huo katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
CHANZO: BBC
MOROCCO YAREJEA RASMI UMOJA WA AFRIKA
Reviewed by Unknown
on
05:53
Rating:
No comments: