RAIS MAGUFULI AKUBALI MKUU WA WILAYA KUJIUZULU
Na Mtapa Wilson
Rais John
Magufuli amelikubali ombi la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyuwi, Mkoani Tabora,
Gabriel Simon Mnyele, ambaye aliomba kujiuzulu wadhifa wake huo kwa hiari yake
mwenyewe hapo jana.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema
kuwa ombi la Mnyele limekubaliwa na Rais na nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyuwi
itajazwa hapo baadaye.
Mkuu huyo wa
Wilaya alimwandikia barua Rais akiomuomba ajiuzulu wadhifa wake huo jana
Alhamis Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
katika mkutano alioufanya wilayani humo.
Gabriel Simon
Mnyele, alikuwa ni miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais
Magufuli mnamo Juni 26, 2016.
RAIS MAGUFULI AKUBALI MKUU WA WILAYA KUJIUZULU
Reviewed by Unknown
on
18:23
Rating:
No comments: