BENKI YA DUNIA KUTOA DOLA MILIONI 305 UTANUZI WA BANDARI DAR
Na Mwandishi wetu
Kutokana na
matatizo mbalimbali yaliyopo kwenye bandari ya Dar es Salaam, ambayo yamekuwa
yakiigharimu serikali na nchi jirani kiasi cha takribani dola za Marekani
milioni 2.6 kila mwaka, Benki ya Dunia ya Dunia (WB) imesema itatoa dola
milioni 305 kama mkopo, kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.
Bandari hiyo
iliyoko katika jiji la Dar es Salaam, ndiyo inayoziunganisha nchi za Afrika
ambazo hazipakani na bahari ya Hindi ikiwemo Zambia, Rwanda, Malawi, Burundi,
Uganda na pia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).
Hatua hiyo
imekuja kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa mwaka 2014 na
kubainisha matatizo mbalimbali kwenye bandari ya Dar es Salaam na kwamba fedha
hizo zitakwenda kusaidia kumaliza matatizo hayo, ambayo yalikuwa yakiigharimu
kiasi kikubwa cha fedha serikali pamoja na nchi nyingine zinazotegemea bandari
hiyo.
BENKI YA DUNIA KUTOA DOLA MILIONI 305 UTANUZI WA BANDARI DAR
Reviewed by Unknown
on
14:55
Rating:
No comments: