RAIS DONALD TRUMP AANZA KUWATIMUA WAAFRIKA
Rais wa Marekani, Donald Trump. |
Marekani
Watu wapatao
92 wakiwamo raia 90 wa Somalia na wengine wawili wa Kenya, wamefurushwa kutoka nchini
Marekani kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wanaishi nchini humo
kinyume cha sheria.
Kwa mujibu
wa Msemaji wa serikali ya Kenya, Eric Kiraithe, tayari watu hao wameshawasili
katika uwanja wa Kimataifa ya Jomo Kenyatta, jijini Nairobi na raia wa Somalia
watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.
“Ni watu 90
kulingana na habari ambazo tumepewa. Wakati
unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu. Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa
inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),” amesema
Kiraithe.
Hatua hiyo
imekuja siku chache mara baada ya Rais Donald Trump kuapishwa rasmi kuwa Rais wa
nchi hiyo, ambapo amesema jumatano ya leo itakuwa ni siku muhimu kwa usalama wa
Marekani, ambapo pia inatarajiwa kuwa ataweka masharti makali kwa raia wa
Mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu
wanaotafuta viza za kwenda Marekani.
Mataifa saba
ambayo yanayotajwa kuwekewa masharti magumu kwa raia wake kuingia nchini
Marekani ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.
Wakati wa
kampeni zake za Urais, Donald Trump, aliahidi kufanyia mageuzi suala la
uhamiaji nchini Marekani ikiwemo kuruhusu ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na
Marekani kwa ajili ya kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu
kuingia katika Taifa hilo ikiwa ni sehemu yake ya kupambana na vita dhidi ya
ugaidi.
CHANZO: BBC
RAIS DONALD TRUMP AANZA KUWATIMUA WAAFRIKA
Reviewed by Unknown
on
15:52
Rating:
No comments: