GAZETI LA MWANAHALISI LAMUOMBA RADHI JPM
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd, inayochapisha gazeti la Mwanahalisi pamoja na gazeti la Mseto, ambalo limefungiwa kwa kipindi cha miaka mitatu, leo imeomba radhi kufuatia kitendo chake cha kuchapisha habari inayoelezwa kuwa ni ya uzushi kupitia gazeti lake la Mwanahalisi.
Habari hiyo iliyochapishwa na Mwanahalisi iliandikwa kichwa cha habari kinachosomeka kuwa “UFISADI NDANI YA OFISI YA JPM”, wakati habari ilihusu ufisadi uliofanyika katika Shirika la Elimu Kibaha na siyo Ikulu kwa Rais Magufuli.
Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Serikali ya Habari Maelezo, ililitaka gazeti hilo kuomba radhi ndani ya saa 24, vinginevyo hatua kali za kisheria zingechukuliwa.
Mwanahalisis imewahi kuonywa mara kadhaa kutokana na tuhuma za uchapishaji wa habari mbalimbali zinazodaiwa kuwa ni uzushi pamoja na uchochezi.
Mwaka 2012, gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa kwa muda usiojulikana ila baadae lilikata rufaa na kushinda kesi mwaka 2015, ambapo lirejea tena mtaani baada ya kutoendeshwa katika kipindi cha miaka mitatu.
GAZETI LA MWANAHALISI LAMUOMBA RADHI JPM
Reviewed by Unknown
on
17:34
Rating:
No comments: