ANNE KILANGO MALECELA ATEULIWA KUWA MBUNGE
Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni takribani miezi tisa tangu Rais John Magufuli kutengua
uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, kutokana na
kile kilichoelezwa kuwa alitoa taarifa za uongo juu ya uwepo wa watumishi hewa
mkoani humo, leo Rais Magufuli amemteua tena Malecela kuwa Mbunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es Salaam imesema kwamba Anne Kilango
Malecela, ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
April, 2016, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa
viongozi wa Mkoa wa Shinyanga akiwemo Mkuu wa Mkoa, Anne Kilango Malecela
(wakati huo) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdul Rashid Dachi, kufuatia kutoa taarifa
za uongo kuwa Mkoa huo hauna watumishi hewa.
Mbali na kuteuliwa kuwa Mbunge tena wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Malecela amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki
na pia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika serikali ya
awamu ya nne.
ANNE KILANGO MALECELA ATEULIWA KUWA MBUNGE
Reviewed by Unknown
on
20:51
Rating:
No comments: