MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA KUNYIMWA MSAADA NA MAREKANI
Marekani
Ni wiki yake
ya kwanza ofisini tangu alipoapishwa rasmi ijumaa wiki iliyopita, kuwa Rais wa
Marekani, Donald Trump, ameanza kazi katika Ikulu ya Marekani kwa kuvunja
mikataba ya Mexico City na TPP.
Rais Trump
amevunja mkataba wa Mexico City, ambao ulikuwa unaruhusu serikali ya Marekani
kutoa fedha kwa mashirika yake mbalimbali ulimwenguni yanayojishughulisha na
masuala ya uzazi wa mpango.
Awali Marekani
ilikuwa ikitoa fedha zake kwa makundi na mashirika ya kimataifa ambayo yalikuwa
yanazitumia kushughulikia ama kujadili utoaji mimba kama njia mojawapo ya uzazi
wa mpango.
Vilevile Rais
Trump ameiondoa nchi yake kwenye Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi
zinazounganishwa na bahari ya Pasifiki. Makubaliano
ya Mpango wa Kibiashara wa nchi zinazounganishwa na bahari ya Pasifiki (TPP),
yalijadiliwa na utawala wa Rais aliyemaliza muda wake, Barack Obama.
Taarifa iliyotolewa
na Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sean Spicer, imesema kwamba hatua hiyo
iliyochukuliwa na Rais ni ishara kabisa ya kuanza kwa enzi mpya ya sera za
kibiashara ya Marekani, ambazo zitakuwa na masilahi mapana kwa Marekani,
kwakuwa zitaongeza ushindani wa wafanyakazi wa Marekani pamoja na uzalishaji.
CHANZO: BBC
SWAHILI
MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA KUNYIMWA MSAADA NA MAREKANI
Reviewed by Unknown
on
07:34
Rating:
No comments: