MASHUSHU WA MAREKANI NA KENYA WAUWAWA NA AL-SHABAB
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabab |
Somalia
Kundi la
kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia limewaua watu watatu kwa kile linachodai
kuwa walikuwa wanalisaidia Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) pamoja na
vitengo vyake vingine kulipeleleza kundi hilo.
Watu waliobainika
na Al-Shabab kuwa walihusika moja kwa moja kuwachunguzia Maofisa wa Ujasusi wa
Marekani na Kenya juu ya mtandao wa kundi hilo, hali iliyosababisha
mashambulizi kadha kutekelezwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani ni Abdullahi
Damey Mohamoud Nur (36), ambaye alikuwa akipokea mshahara wa dola 200 kila
mwezi.
Mtu mwingine
ni Mohamed Iman Hassan (42), ambaye aliuwawa kwa kuwapelelezea Maofisa wa
Shirika la Ujasusi wa Kenya na alikuwa akilipwa mshahara wa dola 150 na Kenya
kwa kazi hiyo.
Aidha Mohamed
Sharrif Ali (21) ameuwawa kwa kuisaidia Mamlaka ya Jubbaland, ambayo alikuwa
anaikusanyia habari mbalimbali kuhusu kundi hilo.
CHANZO: BBC
MASHUSHU WA MAREKANI NA KENYA WAUWAWA NA AL-SHABAB
Reviewed by Unknown
on
15:39
Rating:
No comments: