RAIS MUGABE KUCHINJA NG'OMBE 150 'BIRTHDAY' YAKE
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe. |
Zimbabwe
Ng’ombe
takribani 150 wanatarajiwa kuchinjwa nchini Zimbabwe ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya sherehe kwa ajili siku ya kuzaliwa kwa Rais Robert Mugabe, ambaye anatimiza
miaka 93 ifikapo Februari 21, mwaka huu.
Idadi hiyo
ya mifugo kwa ajili ya kitoweo inatarajiwa kukusanywa kutoka kwa wakulima wakubwa,
ambao walipatiwa mashamba makubwa na serikali baada ya kuyachukua kwa nguvu
kutoka kwa Wazungu katika maeneo ya Matebeleland.
Sherehe hiyo
ya kuzaliwa kwa Rais Mugabe itafanyika katika eneo la Matobos nje kidogo ya mji
wa Bulawayo na inatarajiwa kuhudhuriwa na wananchi wapatao 100,000.
CHANZO: BBC
RAIS MUGABE KUCHINJA NG'OMBE 150 'BIRTHDAY' YAKE
Reviewed by Unknown
on
12:20
Rating:
No comments: