KAULI 10 ZA RUGE MUTAHABA KUHUSU MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA GROUP

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.  Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Mosi, sisi kama Clouds tulianza tukiwa chumba kimoja na tuna miaka 19. Tulikotoka ni mbali na tunakokwenda tunatarajia kupata usalama zaidi kuliko hali ya kuogofya.

Pili, vijana wa Shilawadu wako katika hali mbaya sana. Wameomba likizo. Bora Sudy Brown ambaye hufunika sura kuliko Isakwisa ambaye hafuniki sura maana anaona jamii inamtazama vibaya.

Tatu, mimi sikukamatwa na polisi isipokuwa nilikwenda kuripoti tu polisi kwa kuwa tukio lilikuwa linahusika na uwepo wa silaha. Hivyo ilikuwa ni lazima nikaripoti polisi.

Nne, sisi kama Clouds ni Radio ya Watanzania. Sisi tunawajibika kwa watanzania. Na tukikosea watanzania watatuwajibisha.

Tano, natoa wito kwa vyombo vya habari vilivyotupigia simu. Namshukuru sana katibu mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, Dada yangu Maria Sarungi kwa simu walizonipigia. Sisi kama wadau wa habari tunaomba tujumuike pamoja kudai uhuru wetu. Katika hili kuna namna ya kuadhibiwa kama wadau wa habari siyo kama alivyofanya mkuu hata kama kuna mahala tulikosea.

Sita, mimi nawakilisha watu wote ambao pia waliokosewa. Kwahiyo siwezi kwenda chumbani au kwenye sebule sehemu tukaelewane tu mimi na wewe tumemaliza.  Hapana!  Ni lazima tuweke heshima kwa kile kilichotokea.

Saba, ni rafiki na amekuwa rafiki. Ikumbukwe Makonda ni rafiki kabla hajawa DC au RC. Mimi simlaumu kwakuwa ni rafiki yangu. Ila namlaumu Makonda kwa kutumia vibaya madaraka yake.

Nane, pamoja na ukweli wa mambo mengi lakini bado tuko katika kutafakari.  Kikubwa zaidi hatutaki kugombana na serikali.  Na kama kuna hatua za kuchukua, tutachukua bila kuathiri jitihada za serikali.

Tisa, kwakweli tulionekana kama kituo cha Makonda.  Lakini wengi wanajua na tunawaambia kiongozi yeyote mwenye ajenda yeyote aje, sisi tutampa nafasi azungumze.  Nasisitiza awe na ajenda ya maendeleo.

Kumi, viongozi wanashindana na wasanii kwenye 'kick' kwa sababu 'social networks' (mitandao ya kijamii) siku hizi imekuwa ni sehemu ambayo kila mtu anapambana kwenye 'kick'.  
KAULI 10 ZA RUGE MUTAHABA KUHUSU MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA GROUP KAULI 10 ZA RUGE MUTAHABA KUHUSU MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA GROUP Reviewed by Unknown on 09:31 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.