BASHE AMTAKA MAKONDA KUOMBA RADHI 'CLOUDS MEDIA'
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe. |
Na Mtapa Wilson
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuomba radhi kituo cha habari cha Clouds Media, kwa kitendo chake cha kuvamia kituo hicho akiwa na askari wenye silaha, hali iliyozua taharuki kituoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Bashe amesema kuwa licha ya kufanya kazi vizuri, Makonda tangu akiwa Mkuu wa Wilaya amekuwa akifanya makosa ya kimkakati kila kukicha, hali inayomharibia uhalali wa kukubalika kama kiongozi kwa umma.
“…..kistaarabu Paul Makonda anawajibu wakuomba radhi Clouds kwa kitendo chake cha kungia na askari wenye silaha na kutengeneza taharuki hii. Ni wajibu wa kiongozi yeyote anapokosea kuomba radhi,” amesema Bashe.
Makonda anatuhumiwa kuvamia Clouds Media, siku ya Ijumaa usiku, wiki iliyopita, akiwa na askari wenye silaha kwa madai ya kushinikiza watangazaji wa kituo hicho kurusha kipindi, jambo ambalo linakiuka miiko na maadili ya uandishi wa habari.
BASHE AMTAKA MAKONDA KUOMBA RADHI 'CLOUDS MEDIA'
Reviewed by Unknown
on
16:38
Rating:
No comments: