JPM AMTEUA MKE WA KIKWETE KUWA MBUNGE
Mama Salma Kikwete. |
Na Mwandishi wetu
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amemteua mke wa Rais
mstaafu awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema
kuwa Mama Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu
zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo
awali taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilieleza
kuwa Mama Salma Kikwete ameteuliwa kama Mbunge wa viti maalumu lakini baadaye taarifa hiyo ilisahihishwa na kueleza kuwa ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na mamlaka aliyonayo Rais ya kuteua
wabunge kumi kwa mujibu wa katiba.
JPM AMTEUA MKE WA KIKWETE KUWA MBUNGE
Reviewed by Unknown
on
20:24
Rating:
No comments: