NAPE NNAUYE AWEKWA PEMBENI BARAZA LA MAWAZIRI
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. |
Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, aliyoyafanya leo Machi 23, katika ofisi za Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika mabadiliko hayo, Dk Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema kwamba uteuzi uliofanyika unaanza kutekelezwa mara moja na wateule wote wataapishwa kesho ijumaa Machi 24, mchana katika Ofisi za Ikulu jijini Dar es Salaam.
NAPE NNAUYE AWEKWA PEMBENI BARAZA LA MAWAZIRI
Reviewed by Unknown
on
06:34
Rating:
No comments: