VODACOM YAZINDUA RASMI UUZAJI HISA KWA UMMA
Na Mtapa Wilson
Kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC leo imezindua rasmi uuzaji wake wa hisa kwa
umma kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ikiwa ni utekelezaji wa Sheria
ya Electroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.
Sheria hiyo inaelekeza
kampuni za simu kumilikisha asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga
na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Akizungumza
katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,
Ian Ferrao, amesema kwamba kampuni yake imeanza rasmi uuzaji wake wa hisa kwa
umma kutokana na matakwa ya sheria.
“Hatua hii
ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza
agizo la kuuza hisa zake kwa umma na inaonyesha jinsi gani ilivyojipanga
kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni,” amesema.
Aidha Ferrao
amesema uuzaji wa hisa kwa umma kupitia Soko la Hisa utazidi kukuza shughuli za
Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwa kuwanufaisha watanzania kiuchumi na
kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kampuni ya
Vodacom Tanzania PLC inatarajia kuuza hisa takribani 560 zenye thamani ya shilingi bilioni
500, ambapo hisa moja itakuwa ikiuzwa kwa shilingi 850.
VODACOM YAZINDUA RASMI UUZAJI HISA KWA UMMA
Reviewed by Unknown
on
18:58
Rating:
No comments: