DK. PETER KAFUMU NA VICKY KAMATA, WABWAGA MANYANGA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
Kutoka kushoto ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalaly Kafumu na Makamu mwenyekiti wake, Vicky Kamata. |
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalaly Kafumu, pamoja
na Makamu Mwenyekiti wake, Vicky Kamata, wote kwa pamoja leo wamemwandikia
barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, wakimuomba
kuchia nafasi zao ndani ya kamati hiyo nyeti.
Hata hivyo, katika
barua zao hawajabainisha moja kwa moja sababu za kufanya maamuzi hayo isipokuwa
wote kwa pamoja wameeleza kufikia maamuzi hayo kwa hiari yao wenyewe.
Lakini pia
wamemshukuru Spika Ndugai kwa ushirikiano mkubwa aliouonyesha kwao kwa kipindi
chote walichokuwa viongozi wa kamati hiyo ndani ya Bunge.
DK. PETER KAFUMU NA VICKY KAMATA, WABWAGA MANYANGA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
Reviewed by Unknown
on
11:48
Rating:
No comments: