WAMILIKI VYOMBO VYA HABARI WATISHWA

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli.








Na Mtapa Wilson

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari, ambavyo vimekuwa vikiandika na kusambaza habari, ambazo amedai kuwa za uchochezi ikiwemo migogoro ya wakulima ya wafugaji kuacha mara moja.

Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Mabalozi wa nchi mbalimbali, Dk. Magufuli amevituhumu vikali baadhi vyombo vya habari nchini kuwa vimekuwa mstari wa mbele kuandika na kuchapisha habari za uchochezi na kuziweka katika kurasa za mbele ama kurusha kwa muda mrefu katika televisheni.

Aidha amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kuwa makini na hali hiyo kwani kama wanafikiri kuwa wana uhuru wa habari lakini si kwa kiwango hicho wanachofikiri.

"Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari kuwa makini na kuchukua tahadhali.  Kama mnafikiri mna uhuru namna hiyo basi si kwa kiwango hicho," amesema Rais Magufuli.
WAMILIKI VYOMBO VYA HABARI WATISHWA WAMILIKI VYOMBO VYA HABARI WATISHWA Reviewed by Unknown on 11:09 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.