ZANZIBAR YAPEWA SIKU 14 KULIPA DENI LA UMEME TANESCO




Na Mtapa Wilson

Shirika la ugavi wa umeme nchini (Tanesco) limetoa siku 14 kwa wale wote wanaodaiwa na shirika hilo vinginevyo wakatiwe huduma ya umeme.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco nchini, Tito Mwinuka, amesema kuwa kuna wizara na mashirika mengi ya serikali yanayodaiwa na Tanesco madeni yanayofikia takribani shilingi bilioni tano huku Shirika la umeme Zanzibar (Zeco) likidaiwa shilingi bilioni 121.

Akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupoza umeme kwa njia ya Kv 132 mkoani Mtwara, siku ya jumapili, Rais Magufuli aliliagiza shirika la Tanesco kuwakatia umeme wadaiwa wote sugu ili lipate fedha za kujiendesha kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
ZANZIBAR YAPEWA SIKU 14 KULIPA DENI LA UMEME TANESCO ZANZIBAR YAPEWA SIKU 14 KULIPA DENI LA UMEME TANESCO Reviewed by Unknown on 13:02 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.