CCM YAMVUA UANACHAMA SOPHIA SIMBA, Dk. Nchimbi na Alhaji Kimbisa waonywa vikali
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba. |
Na Mwandishi wetu
Mwanachama mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CCM Taifa (UWT), Sophia Simba, leo amevuliwa
rasmi uanachama wake ndani ya chama hicho.
Uamuzi huo umekuja wakati wa mkutano mkuu maalumu wa
CCM uliofanyika leo mjini Dodoma, ambapo Sophia Simba ametiwa hatiani kwa
kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkali mwaka
2015.
Aidha CCM imewapa onyo kali wanachama wengine
waliopatikana na hatia ya kukisaliti chama hicho akiwemo Dk. Emmanuel Nchimbi
na Alhaji Adam Kimbisa.
Inaelezwa kuwa wanachama hao watatu wametiwa hatiani
kwa usaliti kutokana na kile kinachoitwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa Urais kupitia CCM kabla
ya kukatwa kwake na kuondoa kwenda kujiunga na Chadema.
CCM YAMVUA UANACHAMA SOPHIA SIMBA, Dk. Nchimbi na Alhaji Kimbisa waonywa vikali
Reviewed by Unknown
on
14:20
Rating:
No comments: