WAZIRI NAPE AUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI UVAMIZI 'CLOUDS MEDIA GROUP'

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Na Mtapa Wilson

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameunda kamati ya watu watano ili kuchunguza suala linalodaiwa kuwa ni uvamizi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika kituo cha habari cha Clouds Media Group, siku ya ijumaa usiku wiki iliyopita.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Waziri Nnauye, kufanya ziara katika kituo hicho cha habari leo na kuzungumza na uongozi kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kuvamia kituo hicho akiwa askari wenye silaha za moto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imesema kuwa kamati iliyoundwa itafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kutoka pande zote mbili kisha hatua zaidi kuchukuliwa.

Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, Mhariri Mtendaji gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu, Mengida Johannes kutoka Wapo Redio, na Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).
WAZIRI NAPE AUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI UVAMIZI 'CLOUDS MEDIA GROUP' WAZIRI NAPE AUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI UVAMIZI 'CLOUDS MEDIA GROUP' Reviewed by Unknown on 14:58 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.