ALIYEMTOLEA BASTOLA NAPE NNAUYE MATATANI
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba. |
Na Mtapa Wilson
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, kumsaka na kumkamata haraka mtu mmoja ambaye ameonekana katika picha mbalimbali zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akimwelekezea bastola Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye.
Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wake wa kijamii wa 'facebook', Mwigulu amesema kuwa Nape ni si mhalifu bali ni Mtanzania, Mbunge na ni mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), hivyo kitendo cha mtu kumtolea bastola siyo kitendo cha kiaskari, kitanzania na kicha Mungu.
".......kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini!"
"Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyefanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake,"
Mpaka jana asubuhi, Nape Nnauye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya kuwekwa pembeni hapo kufuatia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyoyafanya Rais wa Tanzania, Dk. Magufuli.
Lakini hata hivyo Nape alitaka kuongea na wanahabari kufuatia uamuzi huo wa Rais ndipo alipovamiwa na mtu huyo, ambaye alimzuia kuongea na wanahabari huku akimwelekezea bastola hadharani akimsihi arudi ndani ya gari lake mara moja.
ALIYEMTOLEA BASTOLA NAPE NNAUYE MATATANI
Reviewed by Unknown
on
06:01
Rating:
No comments: