WAYAHUDI WATUHUMIWA KUMUUA YESU
Mwanasheria, Dola Indidis. |
Na Mwandishi wetu
Dola Indidis ni mwanasheria kutoka Kenya aliyeishtaki
Israel kwa kumuua Yesu Kristo. Anadai
hakuipeleka kesi mahakamani kwa misingi ya kidini bali kwa misingi ya Kisheria.
Yeye anachoangalia si unabii bali bali ni hatua za kisheria.
Pia amesisitiza ameamua kumtetea Yesu kama mtoto wa
Yusufu (fundi seremala) na sio Yesu kama Masihi.
Alipoulizwa mbona ilitabiriwa Yesu atakufa, anasema
anafahamu hilo ila hoja sio Yesu kufa, hoja yake ni mchakato uliyotumika kumuua
haikuwa sawa kisheria. Anadai mahakama
ilikosea kujiingiza kwenye kesi hiyo.
Anasema Yesu ungehukumiwa kifo kwa kufuata taratibu za
kisheria kusingekuwa na shida, ila aliuawa kikatili bila kupewa haki ya
kusikilizwa. Wakati Yesu anapelekwa mahakamani (kwa Pilato) tayari alishaanza
kusulubiwa kabla hata hukumu haijatoka.
Huo ulikuwa ukiukwaji wa sheria maana mtuhumiwa hawezi
kuadhibiwa kabla ya mahakama kujiridhisha kuwa mtu ana hatia. Anasema Yesu angepata wakili wa kumtetea
angeachiwa huru. Hata kama ilimpasa kufa
angeuawa kwa namna nyingine.
Anadai pia Pilato hakuwa na nguvu ya kisheria ya
kusikiliza ile kesi na hata yeye alikiri hilo ndio maana akawarudisha wayahudi
kwa Herode. Lakini akalazimishwa kutoa
hukumu kwa shinikizo la mfalme Herode.
Pia anadai Pilato alikiri Yesu kutokuwa na hatia,
lakini bado alisulubiwa. Sasa kama
Pilato ndio alikuwa Jaji na hakuona hatia ya Yesu kwanini bado Wayahudi walimsulubisha?
Akaongeza kuwa kitendo cha Wayahudi kumsulubisha Yesu
mbele ya Jaji (Pilato) ni kujichukulia sheria mkononi na ni uvunjifu wa haki za
binadamu.
Anadai misingi ya haki ilikiukwa katika kuongoza kesi
(miscarriage of Justice) na Yesu hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alikuwa
akilalamika.
Amesema pia kuwa maamuzi hayakuzingatia kanuni za haki
ya asili (principle of natural justice), na hukumu inapaswa kurekebishwa na
Israel kuomba msamaha.
Ametumia kesi ya Mwai Kibaki vs Daniel Arap Moi yam
waka 1999 kama sehemu ya marejeo ya kesi yake (MWAI KIBAKI Vs DANIEL TOROITICH
ARAP MOI, Case Number :Civ App 172 of 1999").
Mwanasheria huyo anaungwa mkono na makanisa kutoka
nchi za Norway, Marekani, Israel, Uingereza, Tanzania, Afrika Kusini, Canada na
Ujerumani.
WAYAHUDI WATUHUMIWA KUMUUA YESU
Reviewed by Unknown
on
12:00
Rating:
No comments: