MAKONDA 'KUSHNEI', SASA MARUFUKU KUANDIKA WALA KUTANGAZA HABARI ZAKE
Katibu Mkuu wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena. |
Na Mtapa Wilson
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa habari wa Dar es Salaam (DPC), wameazimia kwa pamoja kuanzia leo kutokuandika wala kutangaza habari zote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Hatua hiyo imekuja kutokana na kitendo cha Mkuu huyo wa Mkoa, kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media ijumaa usiku, wiki iliyopita, huku akiwa ameambatana na askari wenye silaha ili kulazimisha kurushwa hewani kwa kipindi cha televisheni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa leo na TEF pamoja na DPC, imesema kuwa utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja kwa vyombo vyote vya habari nchini, na utaendelea hadi pale itakapotangazwa au kuamriwa vinginevyo.
MAKONDA 'KUSHNEI', SASA MARUFUKU KUANDIKA WALA KUTANGAZA HABARI ZAKE
Reviewed by Unknown
on
09:35
Rating:
No comments: