CHADEMA YAFUNGUKA KUKAMATWA TUNDU LISSU
Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. |
Na Mwandishi wetu
Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vicent Mashinji, amesema
kuwa kwa sasa Taifa linaendeshwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na
utawala wa sheria, ambapo viongozi waliopewa dhamana wameamua kusigina katiba
kwa matakwa yao binafsi.
Dk. Mashinji
ametoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wakati
akitoa tamko la chama chake kuhusu kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata
Mwanasheria wa chama hicho na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Amesema mpaka
sasa Jeshi la Polisi limeshindwa kubainisha makosa yaliyosababisha Mbunge huyo
kukamatwa na kukimbizwa haraka makao makuu ya polisi, jijini Dar es Salaam kutoka
mjini Dodoma, ambako alikuwa anahudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea hivi
sasa.
“Kinachofanyika
hivi sasa ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala wa sheria. Haiwezekani na wala haingii akilini Mbunge
mwenye dhamana ya kuwakilishi wananchi ndani ya Bunge akamatwe bila kosa."
"Tumekwenda polisi
leo asubuhi kumuona lakini hakuna kosa analoshitakiwa nalo. Badala yake Polisi wanamtaka atoe maelezo
yake aliyoyatoa wakati akiwa katika jimbo la Dimani, mjini Zanzibar,” amesema Dk.
Mashinji.
Tundu Lissu
alikamatwa na Jeshi la Polisi siku ya jumatatu wiki hii akiwa anatoka
kuhudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma, lakini hata hivyo haikuwekwa wazi sababu
ya kukamatwa kwakwe.
CHADEMA YAFUNGUKA KUKAMATWA TUNDU LISSU
Reviewed by Unknown
on
15:52
Rating:
No comments: