'VALENTINE'S DAY' YATAJWA KUCHOCHEA NGONO
Indonesia
Mamlaka katika baadhi ya maeneo nchini Indonesia
wamepiga marufuku wanafunzi kusherekea siku ya wapendanao wakisema sherehe hizo
zinachochea vijana kujihusisha na vitendo vya ngono kiholela.
Katika
mji wa Makassar, polisi walivamia majumba ya starehe na kuharibu mipira ya
'Condom' iliyowekwa kwa wazi.
Meya
wa mji huo amesema kwamba mipira ya 'Condom', iliondolewa maeneo ya wazi baada
ya wateja kulalamika na kusema inapatikana lakini haiwekwi wazi.
Katika
mji wa pili mkubwa wa Surabaya, wanafunzi wameonywa dhidi ya kusherekea siku ya
wapendanao na maafisa wa serikali ambao wamesema sherehe kama hiyo ni kinyume
cha maadili ya jamii.
CHANZO:
BBC
'VALENTINE'S DAY' YATAJWA KUCHOCHEA NGONO
Reviewed by Unknown
on
17:18
Rating:
No comments: