MAHAKAMA YAZUIA POLISI KUMKAMATA MBOWE

Mwenyekiti wa Taifa Chadema, Freeman Mbowe akiongea na Waandishi wa habari.
Na Mwandishi wetu
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imewaamuru Maafisa wa polisi kutomkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchin, Freeman Mbowe, hadi Ijumaa.
Mbowe alikuwa amefika katika mahakama hiyo kufuatilia mwenendo wa kesi ya kikatiba aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Camilius Wambura.
Katika kesi hiyo, mbali na mambo mengine, Mbowe anapinga amri ya Makonda ya kutaka akamatwe na pia kile alichokiita kudhalilisha watu wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotaja majina ya watu wanaodaiwa kuhusika katika ulanguzi na matumizi ya dawa za kulevya.
Kesi hiyo iliahirishwa mpaka saa saba mchana ambapo walipoingia mahakamani kwa mara nyingine, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliamuru Jeshi la Polisi kumkamata Freeman Mbowe hadi Februari 23, ambapo maombi yake yatakaposikilizwa.
Mahakama imeliambia Jeshi la Polisi kwamba linaweza kumuita Freeman Mbowe kwa mahojiano kama litaona umuhimu wa kufanya hivyo, lakini hawaruhusiwi kumkamata.

MAHAKAMA YAZUIA POLISI KUMKAMATA MBOWE MAHAKAMA YAZUIA POLISI KUMKAMATA MBOWE Reviewed by Unknown on 15:59 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.