RAIS MAGUFULI: VITA DAWA ZA KULEVYA INAHUSU SERIKALI NZIMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. |
Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John
Magufuli amesema kuwa kampeni dhidi ya dawa za kulevya si kampeni ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, peke yake bali ni kampeni ya serikali nzima.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es
Salaam wakati akimuapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali
Venance Mabeyo, ambapo amesema katika kampeni hiyo hakuna atakayepona.
Amesema hata kama mtoto wa Rais anahusika nae
akamatwe, hata kama mke wake anahusika nae akamatwe.
Aidha Rais Magufuli ameshangazwa na kitendo cha mmoja
wa watu waliokamatwa na dawa za kulevya huko kusini mwa Tanzania mpaka sasa haijukikani kesi yake ilipofikia.
Vilevile Rais Magufuli, amempongeza Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, kwa kuwasimamisha kazi askari polisi 12
waliotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara ya dawa za kulevya.
Rais Magufuli amemwambia IGP Mangu, kama angekuwa
hajawasimamisha kazi askari polisi hao mpaka sasa basi yeye ndiyo angemtumbua.
RAIS MAGUFULI: VITA DAWA ZA KULEVYA INAHUSU SERIKALI NZIMA
Reviewed by Unknown
on
09:10
Rating:
No comments: