KINARA WA ULANGUZI MIHADARATI AKAMATWA

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto.
Mexico

Kikosi maalum cha kupambana na biashara ya mihadarati nchini Mexico kimemtia nguvuni kinara mmoja wa genge la Beltran Leyva, ambalo hujishughulisha na ulanguzi wa mihadarati katika eneo la Nuevon Leon, kaskazini mwa nchi hiyo.

Kinara huyo ni  Eleazar Palomo Castillo, maarufu kwa jina la El Cochi au The Pig, ambaye anatajwa kuwa kama kiongozi mkuu wa mihadarati katika mji wa San Pedro Garza Garcia, na kamanda msaidizi wa wa genge hilo katika jimbo hilo linalopakana na Marekani.

El Cochi, alikamatwa na vikosi vya Mexico baada ya gari lake kukataa kusimama katika kizuizi kimoja cha ukaguzi karibu na uwanja wa ndege wa Monterrey nchini humo.

CHANZO: BBC


KINARA WA ULANGUZI MIHADARATI AKAMATWA KINARA WA ULANGUZI MIHADARATI AKAMATWA Reviewed by Unknown on 13:10 Rating: 5

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.