KAMANDA SIRRO: WANAOSHANGAA 'CENTRAL' TUTAWASHUGHULIKIA NA 'TUTAWAGONGA'
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro. |
Na Mtapa Wilson
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, amepiga marufuku
kuanzia leo kitendo cha wananchi kwenda kituo kikuu cha polisi maarufu kama 'central' na kukusanyika
hovyo nje ya kituo hicho bila kuwa na sababu maalum ikiwemo kuwashangaa watuhumiwa
wa mihadarati wanaofika kituoni hapo.
Kamishna Sirro,
amesema tabia ya wananchi kukusanyika nje ya kituo kikuu cha polisi imekuwepo
tangu kuanza kwa zoezi hilo (juma moja lililopita) la kuitwa kwa watuhumiwa wa
biashara na matumizi ya mihadarati, jambo ambalo amelieleza kama tishio kwa
usalama wa wananchi wenyewe na Jeshi la Polisi.
“Kumekuwa na
tabia ya wananchi kuacha shughuli zao na kukimbia kuja kituo kikuu cha polisi. Jueni kwamba kituo cha polisi siyo mahala pa
kuja kupiga soga, siyo mahala pa kuja kutafutia wachumba.”
“Kituo cha
polisi ni mahala unakuja kwa sababu maalum, ukishahudumiwa unaondoka. Sasa inaonekana kuna watu wanakuja wanajazana
kuanzia asubuhi wanakaa wanatafuta chipsi hapahapa na ukimuuliza anachokifanya hata
hajui,” amesema Kamishna Sirro.
Aidha Kamishna
Sirro, amesema kuwa mtu ambaye anatakiwa kuonekana katika eneo hilo la kituo kikuu
cha polisi ni lazima awe na sababu ya msingi, ambapo anapaswa kwenda moja kwa
moja kwenye kitengo cha huduma kwa wateja ndani kituo ili asaidiwe shida yake
badala ya kukaa nje ya kituo akirandaranda hovyo, jambo ambalo litamfanya
achukuliwe hatua kali za kisheria.
“Mahala pa polisi
pana mambo mengi ya serikali. Hatuwezi kuruhusu
mtu yeyote anaingia anazunguka, anajichanganya, anakula chipsi, tutamshughulikia
na tutamgonga kwa mujibu wa sheria,” amesema Kamanda Sirro.
KAMANDA SIRRO: WANAOSHANGAA 'CENTRAL' TUTAWASHUGHULIKIA NA 'TUTAWAGONGA'
Reviewed by Unknown
on
13:28
Rating:
No comments: