CHID BENZ, MR BLUE NA RECHO 'WAMGOMEA' MAKONDA TUHUMA ZA MIHADARATI
Msanii Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz. |
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameliagiza
jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam kuendesha msako mkali dhidi ya
wahutuhumiwa wa uuzaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya ambao wamekaidi
agizo lake la kujisalimisha wenyewe.
Mkuu huyo wa Mkoa, jana alitaja watu ambao wanahusika
na biashara hiyo wakiwamo wasanii wa filamu na muziki wa bongo fleva, ambapo
aliagiza wajisalimishe wenyewe leo katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es
Salaam.
Katika orodha iliyotolewa na Makonda, jana
mbele ya wanahabari ilionyesha idadi ya wasanii nane lakini ambao wamefanikiwa
kujisalimisha leo kituoni ni wasanii wanne tu ambao ni Wema Sepetu, Khalid
Mohamed (TID), Hamidu Chambuso (Nyandu Toz) na Babu wa Kitaa, ambaye pia ni mtangazaji
wa kituo cha televisheni cha Clouds.
Miongoni mwa wasanii ambao walitajwa jana
lakini wamekaidi wito wa Mkuu huyo wa Mkoa ni Rashid Makwilo (Chid Benz), Heri
Samir (Mr Blue) na Winfrida Josephat (Recho), ambapo Makonda ameamuru wasanii
hao kusakwa na kuwekwa rumande kwa kutotii amri yake ya kujisalimisha wenyewe leo kituoni.
CHID BENZ, MR BLUE NA RECHO 'WAMGOMEA' MAKONDA TUHUMA ZA MIHADARATI
Reviewed by Unknown
on
18:59
Rating:
No comments: