11 MBARONI KWA KUKUTWA NA KETE 38 ZA MIHADARATI NA MAGUNIA SITA YA BANGI
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro. |
Na Mtapa Wilson
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kupitia Kamishna Simon Sirro, limesema
kuwa limewakamata watuhumiwa 11 wa biashara ya mihadarati, kete 38 za
mihadarati pamoja na magunia sita ya bangi, katika operesheni yake maalum ya kupambana ili kuitokomeza kabisa biashara hiyo haram.
Kamishna Sirro ametoa
taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, ambapo
amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa ushirikiano wao wa kutoa
taarifa za watuhumiwa hao, ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukamatwa kwao.
“Tunaendelea
vizuri na operesheni dhidi ya wauza dawa za kulevya pamoja na wavutaji wa dawa
hizo. Niseme tu kwamba jana kuna
watuhumiwa 11 wamekamatwa na dawa za kulevya
zipatazo kete 38. Lakini pia
bangi magunia yapatayo sita yamekamatwa. Kwahiyo
operesheni inaendelea vizuri sana.”
"Napenda
kuchukua nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru sana wana Dar es Salaam,
wanaotupa taarifa kuhusiana na uhalifu wa namna hii,” amesema Kamishna Sirro.
11 MBARONI KWA KUKUTWA NA KETE 38 ZA MIHADARATI NA MAGUNIA SITA YA BANGI
Reviewed by Unknown
on
12:03
Rating:
No comments: