CHUO KIKUU CHA LAGOS MARUFUKU NGUO ZA KUBANA
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Lagos nchini Nigeria (Picha na BBC) |
Lagos,
Nigeria
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Lagos nchini Nigeria, wamepigwa
marufuku kuvaa nguo za kubana mwili kutokana na nguo hizo kuonesha sehemu
mbalimbali nyeti za miili yao, jambo ambalo si zuri kwa maadili ya kiafrika.
Tangazo hilo linalokataza hali hiyo limetolewa na uongozi wa chuo
hicho, ambapo limeeleza kuwa wanafunzi wanapaswa kuvaa nguo safi tena
zinazohifadhi vizuri miili yao badala ya kuwaonesha sehemu nyeti za miili yao
kama vile kifua, tumbo, matiti na makalio.
Tatizo la uvaaji usiokuwa na staha miongoni mwa wanafunzi wa vyuo
vikuu limekuwa likiongezeka siku hadi siku ikiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu
nchini Tanzania, ambapo licha ya kuainishwa kwa misingi na maadili ya uvaaji katika
vyuo hivyo lakini bado hali hiyo imeendelea kuwepo.
CHANZO: BBC
CHUO KIKUU CHA LAGOS MARUFUKU NGUO ZA KUBANA
Reviewed by Unknown
on
06:08
Rating:
No comments: