WEMA SEPETU NA WENZAKE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MIHADARATI
Nyota wa filamu na Mshindi wa Ulimbwende nchini Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu. |
Na Mwandishi wetu
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,
linawashikilia watu wapatao 17 wakiwamo wasanii maarufu pamoja na askari polisi
wa jeshi hilo waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusika
na uuzaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya
Mkuu huyo wa Mkoa, kuwataja watuhumiwa kadhaa wakiwamo askari polisi, wasanii
wa filamu na muziki wa bongo fleva, ambao wanadaiwa kuhusika na mtandao wa
biashara ya dawa za kulevya, ambapo aliwaomba leo wajisalimishe kituo kikuu cha
polisi, jijini Dar es Salaam.
Kamanda Sirro amesema operesheni ya kuwakamata
watu hao ilianza tangu jana kupitia kikosi maalum kinachohusisha askari polisi
na vyombo vingine vya usalama, ambapo watu watano walitiwa mbaroni na kufikisha
idadi ya watu waliokamatwa hadi leo kufikia 17.
Baadhi ya watu wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mpaka
sasa kwa mahojiano ni nyota maarufu wa filamu na aliyewahi kuwa mshindi wa
ulimbwende nchini mwaka 2006, Wema Sepetu, Khalid Mohamed (TID), Hamidu
Chambuso (Nyandu Toz) na Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Clouds, Babu wa Kitaa,
ambao wameitikia wenyewe wito huo wa Mkuu wa Mkoa.
WEMA SEPETU NA WENZAKE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MIHADARATI
Reviewed by Unknown
on
17:37
Rating:
No comments: