LIPUMBA: SERIKALI ISIKURUPUKE KUPELEKA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WA MIHADARATI
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Prof. Ibrahim Lipumba. |
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Chama
cha Wananchi (CUF) anayepingwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, Prof.
Ibrahim Lipumba amesema kuwa anaunga mkono suala la watuhumiwa wa biashara au
matumizi ya dawa za kulevya kukamatwa.
Prof. Lipumba amesema
hayo leo jijini Dar es Salaam, nje ya Mahakama Kuu, alipokuwa amekwenda kusikiliza
mwenendo wa mgogoro baina yake na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad,
ambapo amesema anaunga mkono suala la watuhumiwa hao kukamatwa na serikali inapaswa
kupongezwa kwa hilo
Aidha Lipumba
aliongeza kuwa, serikali isikurupuke kuwapeleka watuhumiwa hao mahakamani bila kuwa na
ushahidi wa kutosha kwakuwa suala hilo linaweza kuigharimu fedha nyingi serikali katika uendeshaji wa kesi hizo.
LIPUMBA: SERIKALI ISIKURUPUKE KUPELEKA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WA MIHADARATI
Reviewed by Unknown
on
16:42
Rating:
No comments: