POLISI 12 WALIOTUHUMIWA KWA MIHADARATI WASIMAMISHWA KAZI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. |
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa
Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, leo amewasimamisha kazi askari 12 kufuatia
tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye juzi
alitoa orodha inayowataja baadhi ya askari polisi pamoja na wasanii
wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Taarifa iliyotolewa
na Makonda ilisema kuwa askari polisi wamekuwa wakishirikiana na wauza dawa za
kulevya kwa kupewa rushwa, ambapo wamekuwa wakitoa siri za jeshi hilo pindi
linapokuwa likikabiliana na uhalifu huo, jambo ambalo limekuwa likirudisha
nyuma juhudi za serikali za kutaka kuitokomeza kabisa biashara hiyo haram.
Mkuu huyo wa
Jeshi la Polisi, amewataja askari polisi waliosimamishwa kazi leo ili kupisha
uchunguzi kutokana na tuhuma zinazowakabili ni pamoja na PF 14473 SACP
Christopher Fuime, PF 17041 INSP Jacob Hashim Swai, D 3499 D/SGT Steven Apelesi
Ndasha, E 8431 D/SGT Mohamed Juma Haima, E 5204 D/SGT Steven John Shaga, E 5860
D/CPL Dotto Steven Mwandambo, E 1090 D/CPL Tausen Lameck Mwambalangani.
Aidha askari
wengine waliotajwa kusimamishwa kazi ni E. 9652 D/CPL Benatus Simon Luhaza, D.
8278 D/CPL James Salala, E. 9503 D/CPL Noel Masheula Mwalukuta, WP 5103 D/C
Gloria Mallya Massawe na F. 5885 D/C Fadhili Ndahani Mazengo.
POLISI 12 WALIOTUHUMIWA KWA MIHADARATI WASIMAMISHWA KAZI
Reviewed by Unknown
on
15:26
Rating:
No comments: