IRAN: WAMAREKANI SASA RUKSA KUINGIA NCHINI KWANGU
Rais wa Iran, Hassan Rouhani. |
Iran
Iran imefuta agizo lake lililokuwa linakataza raia wa Marekani
kuingia nchini mwake, ikiwa ni mwendelezo wa majibizano yake na kauli ya Rais
Donald Trump wa Marekani, ambaye hivi karibuni aliagiza raia wa Mataifa saba
duniani yenye Waislamu wengi kutoingia nchini mwake.
Mamlaka ya mambo ya kigeni nchini Iran, imesema kuwa hatua hiyo
imekuja kufuatia uamuzi wa Mahakama uliotolewa jana nchini Marekani na kuamuru
kuahirishwa kwa muda agizo la kuwafurusha raia kutoka mataifa hayo saba ikiwamo
Iran.
Uamuzi huo wa Iran, utawawezesha sasa wanamichezo wa kikosi cha
mieleka wa Marekani, ambao awali walinyimwa viza, kuingia Iran kwa ajili ya
kushiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini humo baadaye mwezi huu.
CHANZO: BBC
IRAN: WAMAREKANI SASA RUKSA KUINGIA NCHINI KWANGU
Reviewed by Unknown
on
12:35
Rating:
No comments: