VIGOGO WA MIHADARATI KUTAJWA TENA LEO
Na Mtapa Wilson
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo saa nne asubuhi anatarajiwa kutangaza
orodha nyingine ya majina ya watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara au
matumizi ya mihadarati.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Makonda kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram,
inasema kuwa awamu ya tatu ya kutaja majina hayo imeshakamilika na ataitaja leo
katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Hii itakuwa
ni mara ya tatu wa Mkuu huyo wa Mkoa kutangaza hadharani majina ya watu
wanaotuhumiwa kwa mihadarati baada ya ile ya awali kutaja wasanii kisha
kufuatiwa na orodha ya pili iliyotaja watu walioitwa vigogo wa biashara hiyo
nchini, ambapo baadhi ya waliotajwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph
Manji.
VIGOGO WA MIHADARATI KUTAJWA TENA LEO
Reviewed by Unknown
on
04:28
Rating:
No comments: