NDUGU WA RAIS KOREA KASKAZINI AUAWA
Ndugu wa kambo wa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-nam. (AFP) |
Kuala Lumpur, Malaysia
Ndugu wa kambo wa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini, Kim
Jong-un, ameuawa nchini Malaysia, kwa mujibu wa Korea Kusini.
Kim Jong-nam, mwenye umri wa miaka 45, anaripotiwa kulengwa
kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Polisi nchini Malaysia wamethibitisha kwa Shirika la habari
la Reuters, kuwa mwanamume raia wa Korea Kaskazini, ambaye alifariki wakati
akipelekwa hospitalini kutoka uwanja wa ndege ni Kim.
Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya Chosum nchini
Korea Kusini, Kim aliwekewa sumu akiwa uwanja wa ndege na wanawake wawili
wanaoaminiwa kuwa maajenti wa Korea Kaskazini.
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un. (AFP) |
Mwaka 2001, Kim alikamatwa akijaribu kuingia Japan akitumua pasipoti
bandia. Aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kuzuru eneo la burudani la
Disneyland mjini Tokyo.
Kim alikuwa akionekana kama mtu ambaye angemrithi
babake lakini kitendo hicho kilisababisha wao kutofautiana.
Kim Jong-nam ndiye mtoto wa kwanza wa kiume wa Kim
Jong-il, ambaye aliitawala Korea Kaskazini kuanzia mwaka 1994 hadi wakati wa
kifo chake mwaka 2011.
Baada ya nduguye mdogo wa kambo kuchukua uongozi wa
Korea Kaskazini wakati babake alipofariki mwaka 2011, Kim Jong-nam hakuoneka sana
na alitumia muda wake mwingi nje ya nchi hasa Macau, Singapore na China.
Alinukuliwa na vyombo vya habari vya Japan akisema kuwa alipinga
uongozi wa kupokezana.
Pia alinukuliwa na kitabu kimoja mwaka 2012 akisema
kuwa mdogo wake ambaye ni nduguye wa kambo hakuwa na tajriba wa kuongoza.
Kim amekuwa akilengwa ili auawe siku za hapo
nyuma. Jasusi mmoja raia wa Korea
Kaskazini, ambaye alifungwa nchini Korea Kusini mwaka 2012, aliripotiwa kukiri
kuwa alikuwa akipanga njama ya kumuua Kim Jong-nam.
CHANZO: BBC
NDUGU WA RAIS KOREA KASKAZINI AUAWA
Reviewed by Unknown
on
15:35
Rating:
No comments: