KANISA LAPINGA WAUZAJI, WATUMIAJI MIHADARATI KUUWAWA
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte. |
Ufilipino
Kanisa katoliki nchini Ufilipino limepinga kampeni ya Rais wa nchi hiyo, Rodrigo
Duterte, ambayo inalenga kukabiliana na wauzaji pamoja na watumiaji wa dawa za
kulevya nchini humo.
Kanisa limesema kuwa kuna upendeleo mkubwa miongoni mwa watu
wanaouawa baada ya kubainika kuwa ni wauzaji au watumiaji wa dawa hizo za
kulevya.
Mpaka sasa Rais Duterte, ameshaamuru kuuawa kwa kupigwa risasi hadharani maelfu ya watu
wanaosadikiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya pamoja na watumiaji wa dawa za
kulevya nchini Ufilipino, jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele kama ukiukaji
mkubwa wa haki za binadamu.
Ujumbe wa kanisa umesomwa leo jumapili kote nchini Ufilipino.
Lakini hata hivyo ujumbe huo umekuja ikiwa ni siku kadhaa tangu
Rais Duterte, asimamishe kwa muda kampeni yake hiyo, kutokana na ufisadi uliopo
katika idara ya polisi, jambo ambalo analitaja kama kikwazo kinachohujumu juhudi
zake za kumaliza kabisa biashara ya mihadarati nchini mwake.
CHANZO: BBC
KANISA LAPINGA WAUZAJI, WATUMIAJI MIHADARATI KUUWAWA
Reviewed by Unknown
on
13:57
Rating:
No comments: