CHADEMA YANG'AKA MBOWE KUTAJWA DAWA ZA KULEVYA
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe. |
Na Mwandishi wetu
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia Katibu Mkuu, Dk. Vicent Mashinji, kimelaani
vikali kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama mmoja wa vigogo wanaotuhumiwa
kwa biashara ya mihadarati.
Akijibu swali
lililoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo, ambaye alitaka
kujua ni ipi kauli ya chadema kuhusiana na orodha iliyotolewa na Makonda ambayo
ndani yake jina la Mwenyekiti wa chama hicho limetajwa.
Dk. Mashinji
amesema kuwa kitendo hicho ni mwendelezo wa hujuma dhidi ya upinzani, ambapo
toka mwanzo viongozi wa ngazi za juu serikalini walinuwia kuumaliza kabisa
upinzani kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020.
“Suala hili
ni tuhuma za mtu binafsi. Ila kitu
ambacho naweza kusema ni kwamba, tunalaani sana kitendo hiki kwakuwa ni udhalilishaji
mkubwa wa Mwenyekiti wetu, ambaye ni Kiongozi Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani
Bungeni, nafasi ambayo ni sawa na Waziri Mkuu.”
“Kumtaja kwa
namna hiyo bila kuwa na ushahidi dhahiri ni kumdhalilisha. Toka serikali hii imeingia madarakani
imeshafanya mambo mengi kwa Mbowe na kila mtu anajua. Ila ninachoamini na jinsi ninavyomfahamu
Mbowe ataendelea kusimama imara kama alivyosimama imara tangu awali. Katika suala hili ninaamini kabisa Mbowe
mwenyewe atalieleza,” amesema Dk. Mashinji.
Leo Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa orodha mpya ya watu 65, ambao
wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya mihadarati, ambayo ndani yake amewataja
wanasiasa na wafanyabiashara maarufu pamoja na kiongozi wa kiroho wa kanisa la
Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima.
CHADEMA YANG'AKA MBOWE KUTAJWA DAWA ZA KULEVYA
Reviewed by Unknown
on
16:52
Rating:
No comments: