MAHAKAMA YARUHUSU WAISLAMU KUINGIA MAREKANI
Rais wa Marekani, Donald Trump. |
Marekani
Mashirika ya
ndege mbalimbali sasa yataanza kubeba abiria kutoka Mataifa saba yenye Waislamu wengi,
ambayo awali raia wake walipigwa marufuku kuingia Marekani.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Idara ya Forodha ya Marekani, ambayo imeruhusu sasa abiria kutoka
Mataifa hayo saba kuingia nchini Marekani.
Hali hiyo
imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Jaji wa Mahakama ya Taifa ya Marekani kuzuia
amri ya Rais Donald Trump, ambaye alitaka raia wa Mataifa hayo saba, ambayo
yana Waislamu wengi kutoingia nchini mwake.
Mahakama iliamua
kuwa Rais Trump, alivunja katiba, ambayo inakataza dini moja kupendelewa kuliko
dini nyingine.
Lakini hata
hivyo serikali imesema itakata rufaa kupinga hukumu hiyo ya Mahakama kwani Rais
Trump ameendelea kusisitiza kuwa hatua yake hiyo imekusudia kuwalinda
Wamarekani.
Mataifa saba
ambayo raia wake walizuiliwa kuingia Marekani ni Syria, Iraq, Iran, Libya,
Somalia, Sudan na Yemen.
CHANZO: BBC
MAHAKAMA YARUHUSU WAISLAMU KUINGIA MAREKANI
Reviewed by Unknown
on
18:36
Rating:
No comments: