SERIKALI YAIONYA MWANAHALISI
Mwandishi wetu
Serikali imelionya
gazeti la Mwanahalisi kutokana na kitendo chake cha kuchapisha taarifa
zinazodaiwa kuwa ni uzushi na kuahidi kuwa itachukua hatua kali zaidi endapo
gazeti hilo litaendelea na uandishi huo unaokiuka maadili ya kitaaluma pamoja
na sheria za nchi.
Hatua hiyo
imekuja siku moja baada ya gazeti hilo kuomba radhi kwa kitendo chake cha
kuchapisha habari iliyokuwa inasomeka kuwa “UFISADI NDANI YA OFISI YA JPM”, jambo
lililotafsiriwa kama kumuhusisha Rais Magufuli na ufisadi huo, wakati habari
ilikuwa inahusu ufisadi uliofanyika katika Shirika la Elimu Kibaha.
Aidha
taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Abbasi,
imemuagiza Mhariri wa Mwanahalisi, Jabir Idrissa, kuchapisha barua yake ya
kuomba radhi katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo katika toleo lijalo la Februari
6, 2017, kwakuwa habari husika ilichapishwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti
hilo toleo lililopita.
SERIKALI YAIONYA MWANAHALISI
Reviewed by Unknown
on
15:23
Rating:
No comments: